MADAI! Mwanaume
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Severin Daniel Ndauka amejitokeza
katika Ofisi za Global Publishers na kudai kwamba, staa wa sinema za
Bongo, Rose Donatus Ndauka ni mtoto wa kaka yake ambaye alichukuliwa
kutoka Tanga na kupelekwa jijini Dar.
Mzee huyo aliyekuwa akizungumza kwa
kujiamini mbele ya waandishi wetu, alisema mwaka 1979, shemeji yake,
Nyazimbili au mama Godwin (anayedaiwa ni mama wa Rose) alijifungua mtoto
wa kike katika Kijiji cha Sakura wilayani Pangani, Tanga ambapo kwa
bahati mbaya mama huyo alifariki dunia hivyo mtoto kuchukuliwa na kanisa
ambalo lipo Msimbazi Dar hakutaka kulitaja jina lililomlea mtoto huyo
kwa kuwa familia haikuwa na uwezo.
“Baada ya hapo, hatupata taarifa tena
lakini mimi niliamua kuja Dar kwa ajili ya kumtafuta Rose. Nilikwenda
Msimbazi, nilipofika nikaambiwa Rose alichukuliwa na kituo cha kulea
watoto kilichopo Kurasini. Ilibidi niende Kurasini, kufika nikaambiwa
alichukuliwa na msamaria mwema kwa ajili ya kumlea kama mtoto wake.
“Tangu hapo hatukupata taarifa nyingine
lakini baadaye dada yangu anaitwa Maria Ndauka akanipigia simu, akasema
amemuona Rose kwenye televisheni akiigiza na marehemu Steven Kanumba
ndiyo nimekuja hapa mnisaidie kumpata,” alisema mzee huyo.
Rose alipotafutwa na kuelezwa ishu hiyo,
alisema alizaliwa jijini Dar na si mwaka 79 kama alivyodai mtu huyo na
kwamba katika Kijiji cha Sakura hana ndugu.
Kama kuna Rose Ndauka mwingine, afike
Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar ili
akutanishwe na mzee huyo. Mhariri.
0 comments:
Post a Comment