MAMBO yamezidi kuwa mambo! Kifo
cha aliyekuwa mwongoza filamu za Bongo, George Otieno ‘Tyson’ kimezidi
kuzua mapya, safari hii ikidaiwa ndugu mmoja (jina tunalo) ameingia
mitini na pesa za rambirambi zilizochangwa jijini Dar es Salaam wakati
wa msiba huo.
Kwa mujibu wa chanzo, ndugu huyo
alikabidhiwa mshiko huo kiasi cha shilingi milioni
mbili za Kibongo ambapo aliaminika kwamba baada ya kutua Nairobi, Kenya ambako mwili wa marehemu ulipelekwa kwa mazishi kutoka Bongo, angezikabidhi kwa familia, hasa baba na mama wa marehemu.
mbili za Kibongo ambapo aliaminika kwamba baada ya kutua Nairobi, Kenya ambako mwili wa marehemu ulipelekwa kwa mazishi kutoka Bongo, angezikabidhi kwa familia, hasa baba na mama wa marehemu.
“Yule jamaa amefika Kenya na hakukabidhi
pesa. Wengi waliamini kwamba angezitoa baada ya kumzika marehemu kule
kijijini Siaya, lakini baada ya mazishi tu akachomoka na kurudi Nairobi.
“Mbaya zaidi amezima simu, kwa hiyo hayupo hewani. Kuna uwezekano amerejea Dar es Salaam kwa kuogopa msala wa familia,” kilisema chanzo hicho.
“Mbaya zaidi amezima simu, kwa hiyo hayupo hewani. Kuna uwezekano amerejea Dar es Salaam kwa kuogopa msala wa familia,” kilisema chanzo hicho.
Pichani ni baadhi wa wanandugu,
Monalisa na mwanaye Sonia (kulia wenye mavazi meupe) katika msiba wa
marehemu George Otieno,’Tyson’.
Kikaongeza: “Awali wakati msiba upo Dar,
kuna mtu alimpa shilingi milioni mbili akampe mama wa marehemu Kenya.
Pia kuna michango mingine iliyotolewa pale Leaders Club (Kinondoni)
akakabidhiwa yeye. Na kuna pesa ya kusafiria mtoto mmoja pia akapewa.
“Sasa baada ya kuzika tu, yule mtu
aliyetoa shilingi milioni mbili akapiga simu kwamba na yeye anakwenda
msibani, ndiyo jamaa akaaga haraka na kuondoka.
Yule alipofika akamuuliza mama wa marehemu kama alipewa shilingi milioni mbili, akasema hajapewa, kumbe jamaa aliondoka haraka kwa sababu alijua kitanuka.”
Yule alipofika akamuuliza mama wa marehemu kama alipewa shilingi milioni mbili, akasema hajapewa, kumbe jamaa aliondoka haraka kwa sababu alijua kitanuka.”
Juzi, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta mdaiwa huyo kwa njia ya simu ya mkononi lakini hakuwa hewani kwa muda mrefu.
George Tyson alifariki dunia Mei 30,
mwaka huu kwa ajali ya gari akitokea Dodoma kuelekea Dar. Alizikwa Juni
14, 2014 kwenye Kijiji cha Siaya, Kisumu, Kenya. Mungu ailaze pema
peponi roho yake. Amina.
0 comments:
Post a Comment