
MWENYEKITI wa
Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amekataa katakata
kuwataja wanachama wanaodaiwa ni mashoga ndani ya klabu hiyo ya jijini
Dar.
Akizungumza na Amani juzikati jijini Dar
baada ya kuombwa kuwataja wadaiwa hao, Steve alisema hashindwi
kuyaanika majina yao, bali uongozi wake kwenye chama hicho si kuingilia
mambo binafsi bali kuunganisha umoja na mshikamano kwa ajili ya tasnia
ya filamu za Bongo.
“Hilo suala kila mtu ananiachia mimi
nilizungumzie kwa kukanusha au kuweka majina hadharani ya wanaodaiwa ni
mashoga. Hadi namaliza uongozi wangu sitafanya hivyo,” alisema Steve.
Siku za hivi karibuni baadhi ya vyombo
vya habari viliwahi kuripoti suala la kuwepo kwa mastaa mashoga kwenye
klabu hiyo yenye nguvu ya ushawishi wa fedha mjini.
0 comments:
Post a Comment