Friday, 20 June 2014

EWE MZAZI HOW THIS PAIN!!:MWANAFUNZI ATUHUMIWA KUMBAKA MTOTO WA KAKA YAKE HADI KUMVUNJA MGUU MKOANI MARA

Jeshi la polisi mkoa wa Mara linamshikilia kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi
wa kidato cha 2 katika shule ya sekondari ya Kemoramba wilayani Butiama, baada ya kutuhumiwa kumbaka mtoto wa kaka yeke mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi, mkazi wa kijiji cha Nyankanga wilayani Butiama.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara ACP Paul Kasabago, amesema kuwa mtoto huyo alibakwa hadi kuvunjwa mguu wake wa kushoto.


Mama mzazi wa mtoto huyo Bi. Annaberi Waitara, akizungumzia tukio hilo akiwa Hopitali ya Serikali Mkoa wa Mara Musoma, amesema kuwa mtoto wake alibakwa na Shemeji yake huyo baada ya kumuachia wakati alipokwenda kuchota maji kisimani

0 comments:

Post a Comment