
Ilisemekana
kwamba wakati hayo yakiendelea, Mbasha alikuwa nyuma ya nondo za
Mahabusu ya Keko jijini Dar es Salaam ambako alishikiliwa.
Kwa
mujibu wa mtu aliyeambatana na Mbasha alipopata dhamana dhidi ya kesi
yake inayomkabili ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17,
alipofika nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar alipigwa butwaa kukuta
hakuna vitu ndani!
Habari
zilidai kwamba alipowauliza majirani kama walimuona mtu akiingia ndani
walimwambia mkewe (Flora) ndiye alikuwa akiingia na kutoka mara kwa
mara.
Ilielezwa kuwa vitu hivyo vilihamishwa Juni 16 ambapo Mbasha alitoka mahabusu Juni 17, yaani siku moja tu.
KITANDA CHA BEI MBAYA
Baadhi ya
vitu vilivyodaiwa kuchukuliwa nyumbani hapo ni kitanda cha bei mbaya
walichokuwa wakilalia kwenye chumba cha baba na mama huku akimwachia
neti ikiwa inaning’inia.
SUTI ZA MAREKANI
Vingine
ni makochi huku akibakisha sofa ndogo ya mtu mmoja, vitu vyote jikoni na
nguo (suti za bei mbaya, walizonunua wakati wakiwa Marekani).
Pia alidaiwa kukomba vile vidani vyote vya dhahabu.

ZAIDI YA MIL. 13
Ukiacha
zile hati za nyumba, viwanja na mashamba, gharama ya vitu vyote
vilivyochukuliwa ndani ni zaidi ya Sh. milioni 13 za Kitanzania (kama
zile ambazo Wema Isaac Sepetu alizomlipia Kajala Masanja asiende jela).
AMWAGA CHOZI
Baada ya
kukutana na mazingira ya aina hiyo, lilikuwa ni pigo lingine zito kwa
Mbasha ambaye alijikuta akimwaga chozi kwa mara nyingine kwa sababu ya
mkewe Flora aliyedumu naye katika ndoa kwa takriban miaka 12.
Ilidaiwa kuwa, Mbasha aliumia kupita kiasi huku akiomba Watanzania waone ubaya aliotendewa.
AMANI LAPEKUWA CHUMBA HADI CHUMBA
Baada ya
kunyetishiwa ishu hiyo, Amani lilifika nyumbani hapo ambapo lilipata
mwanya wa kuingia ndani ya nyumba hiyo kisha kupekuwa chumba hadi chumba
na kujionea kulivyokuwa kweupe huku madirishani mapazia yakiendelea
kubembea kwa upepo mkali uliopo Dar kwa sasa.
Kimuonekano, nyumba hiyo ilikuwa kama kuna familia ilihama hivyo inahitaji kupangishwa au kuhamiwa na mwingine.
MBASHA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Mbasha kuzungumzia ishu hiyo alikiri kukuta hali hiyo nyumbani kwake baada ya kupata dhamana.
“Nilipofika
nyumbani kwangu nilikuta ufunguo wa nyumba kwa majirani. Niliwauliza
kama kulikuwa na mtu anaingia nyumbani nikaambiwa ni Flora. Kama
mnavyoona kuna vitu vingi vya ndani havipo,” alisema Mbasha.
Alipoulizwa kama ana uhakika kuwa mhusika ni Flora, Mbasha alisema yeye alikuta nyumba nyeupe.
Jitihada
za kumpata Flora hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani haikuwa
hewani juzi Jumanne mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.
TUMEFIKAJE HAPA?
Kabla ya
Mbasha kukabiliwa na kesi hiyo ya madai ya ubakaji wa ndugu wa Flora,
Mei 23 na 25, mwaka huu, tayari kulikuwa na mgogoro wa ndoa. Flora
alishaondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini maeneo ya Sinza jijini
Dar.
NINI KINAENDELEA?
Wakati
kesi ya ubakaji ikiendelea kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar huku
Mbasha akiwa nje kwa dhamana, kuna jitihada zinazoendelea ili warudiane
kwani kashfa hiyo inashusha upako wa huduma yao kwa jamii huku wote
wakiwa tayari kwa suluhu.CHANZO GPL
0 comments:
Post a Comment