duniani imani imekwisha! Ikiwa inakaribia miezi miwili tangu kifo cha msanii wa filamu Bongo, Rachel Leo Haule, vitu vya kutisha vinavyoashiria mambo ya uchawi vimekutwa juu ya kaburi lake, Kinondoni jijini Dar.
Tukio hilo la
kustaajabisha, lilidaiwa kutokea Alhamisi iliyopita katika makaburi ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndugu wa
marehemu mmoja ambaye hakujulikana jina walikuwa kwenye makaburi hayo
wakifanya kumbukumbu mbalimbali ndipo walipokuta ‘madongoloji’ hayo juu
ya kaburi la Recho.
Baada ya mpashaji huyo naye kushuhudia mauzauza hayo alipiga simu
kwenye Ofisi za Global Publishers inayochapisha magazeti pendwa ya
Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani na Ijumaa na kupokelewa na
kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambapo alimweleza mkuu wa zamu
hali ilivyo juu ya kaburi hilo.
toa habari: “Jamani hapo ni Global?”
OFM: “Ndiyo. Tukusaidie?”
Mtoa habari: “Kama mnaweza, njooni kwenye Makaburi ya Kinondoni
haraka sana. Juu ya kaburi la Recho kumewekwa vitu kama vya
ushirikina.” OFM: “Tupe dakika sifuri tu.”
OFM WATINGA NA PIKIPIKI
Kama kawaida mkuu wa zamu aliwatuma mapaparazi wake wanaotumia
pikipiki ziendazo kasi ambao walikwenda mpaka eneo la tukio na kukuta
vitu hivyo ambavyo ni tunguri moja iliyoviringishwa shanga, kitambaa cha
kanga chakavu, manyoya ya kuku, yai moja (huenda likawa viza) na vitu
vingine ambavyo havikujulikana ni nini.
WALINZI WATAFUTWA
Baada ya kujionea vitu hivyo, mapaparazi wetu walikwenda kuwauliza
walinzi wa makaburi hayo kama walikuwa na taarifa hizo.Mlinzi mmoja
aliyeonekana kuwa ni fundi wa kuzungumza lakini bingwa wa uoga, hasa kwa
kuona mauzauza ya kutisha kama hayo ndiye aliyepatikana. Akasema:
“Ah! Hivyo vitu vimetupwa na nani? Kuna watu walikuwa wakitembelea makaburi ya ndugu zao ina maana hawakuviona hivyo vitu?
“Lakini huyo mtu aliyewapigia simu mngemuuliza yeye, anaweza kuwa
aliwaona walioviweka. Mimi siwezi kwenda sasa hivi kwenye hilo
kaburi.”
NDUGU WA MAREHEMU WENGINE
Ingawa mlinzi huyo alishindwa kwenda kushuhudia tukio hilo, lakini
watu waliokuwa wakisafisha makaburi ya ndugu zao walifika kwenye kaburi
hilo kujionea madongoloji hayo.
Miongoni mwa waliofika na kuwa mashuhuda ni mama mmoja aliyedai ni
mlokole wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kimara- Temboni jijini Dar ambaye
alikataa kutaja jina lake.
Mlokole huyo alivikemea vitu hivyo kwa Jina la Yesu kisha akasema
havina tena mamlaka ya kishetani kwa wakati huo na vimebaki kuwa
takataka baada ya kuvipiga Neno la Mungu.
BABU ASEMA NI NDUMBA
Shuhuda mwingine alikuwa ni kijana mmoja aliyekwenda kujengea kaburi
la mteja wake ambaye alishtushwa na mauzauza hayo na kusema hali
inatisha! Baada ya kijana huyo, babu mmoja aliyekutwa eneo hilo alisema
vitu hivyo ni ndumba maarufu sana mkoani Tanga ambapo alisema anaifahamu
ndumba hiyo ambapo wachawi walikwenda kuwangia kaburi hilo na kujaribu
kuivuta nyota ya marehemu.
Babu huyo aliongeza kuwa, wachawi hao walichelewa kwani kwa kawaida
kafara kama hiyo hufanywa siku saba baada ya mwili wa marehemu
kuzikwa.“Mara nyingi nyota za wafu huweza kutumiwa na watu walioko
duniani ingawa wakati mwingine mtumiaji wa nyota hiyo anaweza kupatwa na
madhara makubwa ikiwemo kifo cha ghafla.
“Hawa ni cha mtoto tu, walikuja kulichezea hili kaburi lakini wamechemsha,” alisema mzee huyo.
SAGUDA WA RECHO SASA
Baada ya hapo, mapaparazi wetu walimsaka aliyekuwa mchumba wa
marehemu Recho, George Saguda ambaye alisema wao kama familia hawahusiki
na tukio hilo na kudai hiyo itakuwa ni mipango ya washirikina.Saguda
akaenda mbele zaidi kwa kusema: ”Nitakwenda kukutana na walinzi wa
makaburi wanieleze kinagaubaga kulikoni kaburi la mchumba angu kuchezewa
hivyo.”
0 comments:
Post a Comment